Mitambo ya nyuklia ni mifumo changamano inayotumia mgawanyiko wa atomu kuzalisha joto, ambalo baadaye hubadilishwa kuwa umeme. Usalama na udhibiti ni vipengele muhimu sana kwa kuhakikisha hakuna mionzi inayoathiri mazingira.
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wanafunzi wa Jamiatul-Mustafa (s) - Dar-es-Salaam, Tanzania, leo hii Tarehe (18-08-2025) wameendelea na somo muhimu kuhusiana na Umeme. Somo la leo limehusiana na: "Nuclear Power Plant Components" (Sehemu za Kawaida za Kiwanda cha Umeme wa Nyuklia). Mwalimu wa somo amefundisha kwamba: Kiwanda cha nguvu za nyuklia kinatumia mchakato wa nyuklia ya mgawanyiko (nuclear fission) kuzalisha joto, ambalo hubadilishwa kuwa umeme. Na zifuatazo ndizo sehemu kuu za kiwanda hicho:
1. Reactor Core (Kiini cha Reactor)
Ndipo mgawanyiko wa nyuklia hutokea. Kina fuel rods (yaani: Mishipa ya mafuta ya nyuklia) yenye uranium-235 au plutonium-239. Hapa ndipo joto huzalishwa.
2. Control Rods (Viti vya Kudhibiti)
Hutengenezwa kwa nyenzo zinazonyonya neutroni (kama: Boron au Cadmium). Hudhibiti kasi ya mchakato wa mgawanyiko kwa kupunguza au kuongeza neutroni.
3. Coolant (Kipoza joto)
Kimiminika (kama maji au gesi) kinachopitishwa kwenye reactor kuchukua joto. Kazi yake ni kupoza reactor na kusafirisha joto kwenda kwenye sehemu nyingine ya kiwanda.
4. Steam Generator (Kizalishaji mvuke)
Joto kutoka kwenye coolant hutumika kuyachemsha maji, kutengeneza mvuke wa shinikizo kubwa. Mvuke huu huendesha turbine (iliyoelezwa hapo namba 5).
5. Turbine
Inazungushwa na mvuke wa moto. Mzunguko huu hubadilishwa kuwa nguvu ya umeme.
6. Generator
Inabadilisha nishati ya mzunguko wa turbine kuwa umeme wa kutumia majumbani au viwandani.
7. Condenser (Kipozaji)
Hubadilisha mvuke kuwa maji baada ya kuzungusha turbine. Maji haya hurudishwa kwenye mfumo kutumika tena.
8. Containment Structure (Muundo wa Kudhibiti)
Jengo lenye ukuta mzito linalozunguka reactor. Linalinda mazingira dhidi ya mionzi ya nyuklia na kuzuia ajali kuenea nje.
Kwa Muhtasari:
Mitambo ya nyuklia ni mifumo changamano inayotumia mgawanyiko wa atomu kuzalisha joto, ambalo baadaye hubadilishwa kuwa umeme. Usalama na udhibiti ni vipengele muhimu sana kwa kuhakikisha hakuna mionzi inayoathiri mazingira.
Your Comment